Karani wa bunge aitaka KEPSA kutotumia mahakama kukabili miswada bungeni

Marion Bosire
1 Min Read
Samuel Njoroge, Karani Bunge la Taifa

Karani wa bunge la kitaifa Samuel Njoroge ameomba chama cha sekta ya kibinafsi nchini KEPSA kukoma kutumia mahakama kutatua miswada iliyo bungeni ambayo wanaichukulia kuwa yenye utata.

“Mahakama zinafaa kuwa jawabu la mwisho kabisa kwa KEPSA. Wanafaa kujadiliana na bunge kuhusu masuala hayo. Tuko tayari kuwasikiliza.” Alisema Njoroge.

Aliitaka KEPSA kumakinika na mikataba na mapatano huku wakikusanya maoni ya umma hasa katika sekta ya umma kuhusu sheria zilizopendekezwa.

Alitaja kikao cha Spika wa bunge na wadau wa sekta ya kibinafsi KEPSA kuwa hatua muhimu.

Kiliandaliwa wakati wa mkutano wa mwaka huu wa viongozi wakuu wa bunge katika eneo la Naivasha kaunti ya Nakuru. Mkutano huo unatarajiwa kukamilika kesho.

Share This Article