Kanja: Usajili wa polisi utakuwa wa kuaminika na haki

Tom Mathinji
1 Min Read
Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja.

Inspekta Jenerali wa polisi Douglas Kanja, amesema zoezi la kuwasajili makonstebo wa polisi litatekelezwa kwa njia ya haki na uwazi.

Akizungumza wakati wa mkutano ulioandaliwa katika Chuo cha Mafunzo kwa Maafisa wa Polisi cha Embakasi A Jijini Nairobi, Kanja alisema Huduma ya Taifa ya Polisi, imejitolea kuhakikisha zoezo hilo ni la kuaminika, huku akiwataka maafisa watakaoongoza zoezi hilo kujiepusha na ufisadi.

Akizungumza kwenye mkutano huo, mwenyekiti wa Tume ya Huduma ya Taifa ya Polisi  Dkt. Amani Yuda Komora, alidokeza kuwa tume hiyo, itaunga mkono kikamilifu mchakato huo wa usajili wa maafisa wa polisi, kuhakikisha unaendeshwa kwa njia ya uwazi na uwajibikaji.

Wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Huduma ya Taifa ya Polisi Profesa Collette Suda, Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Eliud Lagat, Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi wa Utawala Gilbert Masengeli na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mohamed Amin miongoni mwa maafisa wengine wakuu wa polisi.

TAGGED:
Share This Article