Inspekta Mkuu wa Polisi Douglas Kanja amewaongoza maafisa wa huduma ya kitaifa ya polisi kwa ibada ya shukrani iliyoandaliwa katika kanisa la Holy Family Basilica.
Ibada hiyo maaluma iliwashirikisha polisi wa utawala, APS, polisi wa DCI, maafisa wa misitu nchini KFS, maafisa wa huduma ya kitaifa ya vijana NYS, maafisa wa shirika la wanyamapori KWS miongoni mwa vikosi vingine.
Kanja aliandamana na manaibu wake Eliud Lagat na Gilbert Masengeli.