Kampuni ya Interscope yasimamisha matangazo yote ya D4vd

Marion Bosire
2 Min Read
Celeste Rivas na D4vd

Kampuni ya muziki ya Interscope inayomsimamia mwanamuziki wa Marekani D4vd imesitisha matangazo yote ya msanii huyo anapoendelea kuchunguzwa kuhusiana na mwili uliopatikana kwenye gari lake.

Haya yanajiri wakati maafisa wa polisi wa Los Angeles wanaendelea kuchunguza uhusiano uliopo kati ya mwanamuziki huyo na binti huyo wa miaka 15 ambaye mwili wake ulikuwa ukioza ndani ya gari lake aina ya Tesla.

Duru zinaarifu kwamba kampuni inayomiliki Interscope ya UMG na ile ua usambazaji wa muziki ya Sony Music zote zimesimamisha mipango ya kutangaza kazi za mwanamuziki huyo.

Chapisho la hivi punde zaidi la D4vd ni la Septemba 7, 2025 ambayo ni tarehe ya kuzaliwa ya msichana huyo kwa jina Celeste Rivas.

Albamu ya D4vd iitwayo “Withered” inatarajiwa kuzinduliwa ijumaa lakini alizindua mikusanyiko miwili ya nyimbo mwaka 2023, mmoja ukiitwa ‘Petals to Thorns’ na mwingine ‘The Lost Petals’ chini ya kampuni ya Interscope.

Haya yanajiri wakati ambapo picha zinaibuka zinazomwonyesha D4vd akiwa na Rivas huku polisi wakifanya msako kwenye nyumba yake kutafuta ushahidi wa damu.

Kati ya picha hizo ni moja iliyopigwa wakati Rivas alikuwa na umri wa miaka 13 pekee na wawili hao wanaonekana kama wapenzi wa dhati.

Mwili wa Rivas ambaye aliripotiwa kutowela Mei 2024 ulipayikana kwenye gari hilo la D4vd lililotwaliwa kwa kutelekezwa pasipofaa mwanzo wa mwezi huu huko Hollywood, California.

D4vd ambaye jina lake halisi ni David Anthony Burke hajashtakiwa rasmi kuhusiana na suala hili.

Share This Article