Waziri wa Ulinzi Soipan Tuya, siku ya Ijumaa katika Makao Makuu ya Vikosi vya Ulinzi, alimuaga Kamanda wa Jeshi la wanaanga Meja Jenerali Fatuma Gaiti Ahmed, ambaye amestaafu.
Meja Jenerali Fatuma Ahmed, amestaafu baada ya kuhudumu jeshini kwa miaka 42, muda ambao alipanda ngazi hadi kuwa mwanamke wa kwanza kuwa na wadhifa wa Meja Jenerali mwaka 2018.
Mwaka 2024, Meja Jenerali mstaafu Fatuma Ahmed, aliweka historia alipoteuliwa mwanamke wa kwanza kuwa kamanda wa jeshi la wanaanga.
Meja Jenerali mstaafu Fatuma Ahmed ni wa kupigiwa mfano kwa wanawake wengi walio katika sekta ya usalama hapa nchini.