Kagame amteua Justin Nsengiyumva kuwa Waziri Mkuu mpya

Nsengiyumva anatwaa nafasi iliyoachwa wazi kufuatia kuondoka kwa Édouard Ngirente, ambaye amehudumu katika wadhfa wa Waziri Mkuu tangu mwaka 2017.

Dismas Otuke
0 Min Read

Rais wa Rwanda Paul Kagame amemteua Dkt Justin Nsengiyumva, kuwa Waziri Mkuu mpya.

Nsengiyumva anatwaa nafasi iliyoachwa wazi kufuatia kuondoka kwa Édouard Ngirente, ambaye amehudumu katika wadhfa wa Waziri Mkuu tangu mwaka 2017.

Nsengiyumva ni mtaalam wa masuala ya uchumi kutoka chuo kikuu cha Leicester, na awali alihudumu kama Naibu Gavana wa benki kuu nchini Rwanda tangu Februari mwaka huu.

Share This Article