Kadinali Robert Prevost ndiye Papa Mpya, achagua jina Leo XIV

Tom Mathinji
1 Min Read
Pope Leo XIV

Kadinali Robert Francis Prevost, amechaguliwa Papa wa 267 wa kanisa Katoliki na kuchagua jina la Papa Leo XIV.

Alichaguliwa na Makadinal 133, waliokusanyka katika kanisa la Sistine kwa mchakato huo ulioanza Jumatano May 7,2025 kufuatia kifo cha Papa Francis.

Papa Leo XIV anaweka historia kwa kuwa raia wa kwanza wa America kuchaguliwa kiongozi wa kanisa Katoliki.

Papa Leo XIV mwenye umri wa miaka 69 ametumia muda wake mwingi akitumikia nchini Peru, na ana uraia wa Marekani na Peru.

Akihutubia umati uliokuwa umekusanyika, Papa huyo mpya alitoa shukrani kwa mtangulizi wake, Papa Francis, huku akisema anataka kuwasilisha baraka zake kwa watu kama Papa Francis alivyofanya mara ya mwisho alipojitokeza katika uwanja wa St Peter’s Square

Katika hotuba hiyo, alizingumza kwa lugha mbili, Kiitaliano na Kiispania.

Mzaliwa huyo wa Chicago, Illinois, mwaka 1955, amehudumu katika Kanisa Katoliki kwa muda wa miongo minne.

Alitawazwa kuwa kasisi Juni 19, 1982 kabla ya kuwa Askofu Disemba 12, 2014.

Kuchaguliwa kwa Papa huyu kunafuatia kifo cha Papa Francis, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 88 siku ya Jumatatu ya Pasaka 21 April, na mazishi yake kufanyika siku ya Jumamosi 26 April.

TAGGED:
Share This Article