Jux kufanya harusi nyingine nchini Nigeria

Hafla hiyo itaandaliwa mwezi Aprili mwaka huu.

Marion Bosire
1 Min Read
Juma Jux na Priscilla Ojo

Mwanamuziki wa Tanzania Juma Jux anatarajiwa kufanya harusi nyingine nchini Nigeria alikozaliwa mkewe Priscilla Ojo.

Mamake Priscilla, Iyabo Ojo ametangaza kupitia Instagram kwamba harusi ya Nigeria itakuwa ya awamu mbili moja ya kitamaduni na nyingine ya kidini.

Hafla hizo zitaandaliwa mwezi Aprili mwaka huu wa 2025 huku hafla ya mwisho kabisa ikitarajiwa kuandaliwa nchini Tanzania mwezi Mei mwaka huu.

“Kwa kila mmoja aliyesafiri kusherehekea ndoa ya binti yangu Priscilla na mwanangu Juma, nitashukuru milele!” aliandika Iyabo Ojo akiongeza kwamba harusi ya wanawe ya Tanzania ya awamu tatu ilifana sana.

“Na tukaishi kushuhudia watoto wetu wakisherehekea hatua muhimu maishani mwao.” aliongeza kusema mama huyo wa watoto wawili.

Juma Jux na Priscilla Ojo walifunga ndoa iliyokuwa na matukio matatu ya siku tofauti nchini Tanzania ambapo walianza na Nikka Februari 7, 2025.

Hafla ya pili Juma aliirejelea kuwa ya kumchumbia tena Priscilla na ilihudhuriwa na watu wa familia yake na marafiki kutoka Nigeria.

Usiku huo alimvisha pete nyingine ya uchumba ambayo alisema ni kubwa na ghali kuliko ya kwanza.

Awamu ya tatu ilikuwa sherehe ya ndoa ambapo Priscilla alivaa gauni la rangi nyeupe huku Juma akivaa suti ya rangi nyeusi.

Share This Article