Timu ya taifa ya wanawake ya Kenya kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 17-Junior Starlets itamenyana kesho alasiri na wenyeji Uganda katika mkondo wa kwanza raundi ya pili kufuzu kwa fainali za kombe la dunia.
Mechi hiyo itapigwa katika uga wa Nakivubo Hamz jijini Kampala, Uganda.
Kenya chini ya ukufunzi wa kocha wa Mildred Cheche, inalenga kufuzu kwa kombe la dunia kwa mara ya pili baada ya kufuzu mwaka jana katika Jamhuri ya Dominika.
Mechi ya marudio itaandaliwa katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex huku mshindi akifuzu kwa raundi ya tatu.