Julius Malema azuiwa kuingia Uingereza

Tom Mathinji
1 Min Read
Julius Malema azuiwa kuingia Uingereza.

Mwanasiasa wa Afrika Kusini anayekabiliwa na utata kuhusiana na mzozo kuhusu ubaguzi wa rangi, amezuiwa kuingia nchini nchini Uingereza.

Afisi ya Mambo ya Ndani ya Uingereza ilisema Julius Malema amekisiwa kutokuwa na nia njema kwa umma, na kwamba hafai kuruhusiwa kuingia nchini humo.

Kupitia barua iliyochapishwa na kituo cha habari katika eneo hilo cha ‘News 24’, serikali ya Uingereza ilitaja usemi wake wa kuunga mkono kundi la Hamas, pamoja na hotuba aliyotoa baada ya shambulizi la Oktoba 7, ambapo alisema chama chake kingetoa silaha kwa kundi hilo iwapo kingechukua mamlaka, kuwa sababu ya hatua hiyo.

Chama chake cha ‘Economic Freedom Fighters (EFF), ambacho kiliibuka cha nne katika uchaguzi wa bunge la Afrika Kusini mwaka jana, kilikashifu uamuzi huo na kuutaja kuwa wa uoga, kikiutaja kuwa kizuizi kwenye mjadala wa kidemokrasia.

Hii ni mara ya pili kwa Malema kukatazwa kuingia Uingereza katika kipindi cha miezi miwili.

TAGGED:
Share This Article