Julia Fox ajutia kufanyiwa upasuaji wa urembo

Mwigizaji huyo alikiri kuanza kupata huduma hizo akiwa mdogo kwa nia ya kuendelea kuvutia wanaume.

Marion Bosire
2 Min Read

Mwigizaji wa Marekani Julia Fox amesema kwamba anajuta kufanyiwa upasuaji wa kuboresha mwonekano wake akiwa na umri wa miaka 21 pekee.

Akizungumza kwenye mahojiano Fox alikiri kwamba aliamini kwamba alistahili kuwa na mwonekano unaovutia wanaume ili aweze kuishi.

Katika mazungumzo hayo Fox alisema ni muhimu kwa mtu maarufu kuwa mkweli ndiposa anafunguka kwamba alianza kufanyiwa upasuaji wa kuboresha mwonekano wake akiwa na umri mdogo.

Fox alisema kwamba kila anapoona mtu ambaye anajua hajawahi kufanyiwa upasuaji kama huo anatamani angerejea nyuma na kuwa kama mtu huyo.

Hii sio mara ya kwanza mwigizaji huyo anazungumzia safari yake ya kuboresha mwonekano wake ambapo alitaja huduma mbali mbali ambazo amepokea kwa ajili hiyo ikiwemo ile ya kuborehsa meno.

Julia ambaye sasa ana umri wa miaka 35, anaonekana kubadili mtazamo wake kuhusu ubreshaji wa mwonekano na mvuto kwa wanaume.
Hapingi uwezekano wa kufanyiwa huduma hizo katika siku za usoni lakini anasema sasa hazipi kipaumbele.

“Huenda nikatafuta huduma hizo siku mpja lakini kwa sasa siwazii” alisema Fox.

Wanawake wengi maarufu hasa wale wa Hollywood huwa wanaogopa sana kuzeeka lakini Fox anasisitiza kwamba mwanamke mwenye umri mkubwa anayezeeka vizuri bila kufanyiwa upasuaji ana uzuri wake.

“Ukiwa mdogo na mwenye mvuto, huo unakuwa utambuzi wako. Halafu sasa unajibidiisha kusalia hivyo” aliendelea kusema mwigizaji huyo.

Share This Article