Jukwaa la Usalama: Waziri Murkomen azuru Meru,Embu na Tharaka Nithi

Tom Mathinji
1 Min Read

Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen, atazuru Mashariki ya juu ya taifa hili katika kaunti za Meru, Tharaka Nithi, and Embu, kukadiria hali ya usalama.

Ziara ya Waziri hiyo itang’oa nanga kwa kushiriki mkutano na kamati ya usalama ya Meru, kabla ya kuzuru kituo cha usajili wa vitambulisho na kampeni dhidi ya mihadarati inayoongozwa na Halmashauri ya kukabiliana na pombe na dawa za kulevya (NACADA).

Aidha Waziri huyo atashiriki misururu ya mikutano na wananchi katika uwanja wa michezo wa Kinoru kuhusu maswala ya usalama.

Mikutano ya Jukwaa la Usalama huhudhuriwa na maafisa wa serikali ya taifa kuanzia kwa kamishna wa kaunti hadi kwa naibu wa chifu, viongozi wa jamii, wafanyabiashara na vijana.

Katika kaunti ya Meru, Murkomen ataangazia upya swala la wizi wa mifugo katika mpaka wa Meru na Isiolo.

Aidha, kaunti ya Meru pia inakabiliwa na mizozo ya muda mrefu ya ardhi, hususan katika mpaka wa Meru na Tharaka Nithi.

Share This Article