Tume ya Huduma za Mahakama nchini (JSC) imewaita watu 598 kwa mahojiano ya nafasi 100 za mahakimu wakazi.
JSC ilikuwa imetangaza nafasi 100 mwezi Juni mwaka huu za Mahakimu Wandamizi na kupokea jumla ya maombi 1,742 kote nchini.
Watakaofaulu watatumwa kuhudumu katika mahakama yoyote nchini.