Tume ya Huduma za Mahakama nchini (JSC) imepuuzilia mbali wito wa Tume ya Usimamizi wa Haki (CAJ), kuwaita wanachama wake kufika mbele yake na kujibu baadhi ya malalamishi dhidi yao.
JSC imesema CAJ imekiuka haki zake na inalenga kuidhalilisha idara ya mahakma nchini ikataja kuwa vitisho na ukiakaji wa haki za wanachama wa JSC.
Mnamo Februari 3 mwaka huu, CAJ ilitaka maelezo kuhusu malalamishi zaidi ya 700 ya usimamizi mbovu dhidi ya wanachama wa JSC.
Msajili Mkuu wa Idara ya Mahakama Winfridah Mokaya amesema JSC kamwe haitatishwa wala kushurutishwa na itasalia kuwa huru na kutekeleza majukumu yake bila uoga wala mapendeleo.
Aidha, Mokaya ameongeza kuwa JSC itachukua hatua zifaazo kulinda uhuru wake.