Bunge la kaunti ya Marsabit leo Jumatano limewahoji wanachama wa jopo la watu watano, litakalowachagua wanachama wa bodi ya Utumishi wa Umma ya kaunti Marsabit.
Jopo hilo la uteuzi lilifika mbele ya kamati ya usaili ya bunge hilo siku ya Jumatano, likiongozwa na Spika Edin Wario Dida.
Waliopigwa msasa ni pamoja na David Dida Wario anayependekezwa kuwa Mwenyekiti wa jopo hilo, Sabdio Roba Okile anayewakilisha sekta ya kibinafsi, John Galimogle mwakilishi wa Taasisi ya Wahasibu nchini ICPAK, Abdilatif Jarso anayewakilisha mawakili na Mariam Challa anayewakilisha Muungano wa Wafanyakazi.
Kamati ya bunge ya upigaji msasa sasa inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake bungeni, ili kuidhinishwa na wawakilishi wadi wote.