JOBO, Agai na Musingu zaonyesha ubabe

Dismas Otuke
1 Min Read

Shule za st, Joseph – JOBO (Bonde la Ufa, Agai Mixed (Nyanza) na Musingu (Magharibi) zimedhihirisha kuwa tishio katika mashindan ya kitaifa ya muhula wa pili baina ya shule za upili yaliyoanza leo jumanne katika kaunti ya Kakamega.

Kwenye mechi za ufunguzi zilizosakatwa katika shule ya wavulana ya Kakamega, JOBO iliwaadhibu mabingwa watetezi Highway mabao matatu kwa moja nayo Agai ikairindima Garissa magoli tisa kwa moja.

Katika uga wa Mumias, wenyeji Musingu walivuna ushindi wa mabao matano kwa moja dhidi ya Moi High Mbiruri.

Vile vile, waakilishi wa eneo la kati – Kirangari walipata ushindi wa mabao mawili kwa nunge dhidi ya waakilishi wa Pwani – Serani.

Katika kitengo cha vipusa, wenyeji Butere waliwapokeza Dr.Charles kichapo cha magoli tano kwa nunge nao Dagorreti wakatoshana nguvu ya magoli mawili kwa mawili na Mwanambeyu.

Wakati uo huo wenyeji wengine – Madira waliwalambisha sakafu Kobala bao moja kwa sufuri.

Matokeo sawia yaliandikishwa na Nasakol dhidi ya Ruiru.

Hapo kesho, Highway watakabana na Kirangari, JOBO wachuane na Serani, Musingu dhidi ya Garissa kisha Agai wahitimishe na Mbiruri

Share This Article