Kamati ya Bunge la Taifa kuhusu Haki na Masuala ya Sheria (JLAC), juma hili itawasilisha ripori yake kuhusu ufaafu wa watu saba walioteuliwa kuwa Makamishna katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).
Ripoti hiyo itawasilishwa baada ya Kamati hiyo kuwasaili makamishna hao siku ya Jumamosi. Aidha wabunge hao huenda wakakubali uteuzi wao rasmi, wapinge orodha hiyo au waifanyie marekebisho.
Mnamo Ijumaa, Jaji Mkuu Martha Koome alibuni jopo la majaji watatu wakiongozwa na jaji Roselyne Aburili, jaji Chigiti Mugwimi na jaji Andrew Mwamuye kuanza kusikiza kesi inayopinga mchakato wa uteuzi wa makamishna hao.
Kesi iliyowasilishwa na wanaharakati Bonface Mwangi na Kelvin Roy kupitia kwa mawakili Paul Muite na Douglas Otieno inahoji uhalali wa kikatiba wa mchakato huo wa uteuzi unaoendelea.