Jepchirchir atwaa dhahabu ya Marathon Tokyo

Kenya na Marekani zinaongoza msimamo wa nishani kwa dhahabu 2 kila moja.

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa wa Olimpiki mwaka 2021 Peris Jepchirchir alishinda dhahabu ya marathon katika mashindano ya Riadha Duniani mjini Tokyo, Japana mapema Jumapili.

Jepchirchir alitimka katika mzunguko wa mwisho akimshinda Tigist Asefa kutoka Ethiopia na kukata utepe kwa muda wa saa 2 dakika 24 na sekunde 43 akishinda dhahabu ya pili kwa Kenya.

Assefa alinyakua medali ya fedha kwa saa 2 dakika 24 na 45 huku shaba ikimwendea Julia Paternain, aliyenyakua nishani ya kwanza ya Uruguay katika historia ya mashindano ya Dunia.

Dhahabu hiyo ilikuwa ya pili kwa Kenya baada ya Beatrice Chebet kunyakua dhahabu ya mita 10,000 siku ya Jumamosi.

Kenya na Marekani zinaongoza msimamo wa nishani kwa dhahabu 2 kila moja.

Share This Article