Jaji wa Mahakama ya Upeo Mohammed Ibrahim amefariki

Tom Mathinji
1 Min Read
Jaji wa Mahama ya Upeo Mohamed Ibrahim ameaga dunia.

Jaji wa mahakama ya upeo Mohammed Ibrahim ameaga dunia.

Akithibitisha kifo hicho, Jaji Mkuu Martha Koome alisema Ibrahim alifariki Jumatano baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Jaji huyo ambaye alitarajiwa kustaasfu Januari 1, 2026, alifariki muda mfupi baada ya saa kumi na nusu alasiri.

Hadi kifo chake, Ibrahim alihudumu katika Idara ya Mahakama kwa muda wa miaka 23.

Jaji Mkuu Martha Koome,  alisema Ibrahim alikuwa mtetezi mkuu wa katiba, mfumo wa haki na heshima ya kibinadamu.

Justice Ibrahim alijiunga na Idara ya Mahakama mwaka 2003 akiwa Jaji wa Mahakama Kuu, kabla ya kujiunga na Mahakama ya Upeo mwaka 2011.

Pia alihudumu wadhifa wa mwenyekiti wa kamati ya Idara ya Mahakama kuhusu Uchaguzi na alikuwa mwakilishi wa Mahakama ya Upeo kwenye Tume ya huduma za Idara ya Mahakama.

Ibrahim amemwacha mke na watoto wanne.

Share This Article