Ivory Coast: Rais Alassane Ouattara kuwania muhula wa 4

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais wa Ivory Coast Allasane Ouattara.

Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara, ametangaza kuwa atawania urais kwa muhula wa 4 kwenye Uchaguzi Mkuu ujao  utakaoandaliwa mwezi Oktoba.

Kwenye hotuba iliyopeperushwa moja kwa moja kupitia televisheni hapo jana, rais huyo mwenye umri wa miaka 83 alisema afya yake na katiba ya nchi inampa nafasi kuwania muhula wa 4.

Ouattara, ambaye alichukua hatamu kama rais tangu mwaka wa 2011, alisema taifa hilo linapitia wakati mgumu kiusalama , kiuchumi na kifedha matatizo ambayo yanahitaji kiongozi mwenye uzoefu.

Tayarai demokrasia nchini humo ipo kwenye njia panda kwani viongozi wa upinzani wanakabiliwa na mtatizo ya kuwazuia kushiriki uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na kiongozi wa cahama cha Democratic Party of Ivory Coast (PDCI) Tidjane Thiam na aliyekuwa rais Laurent Gbagbo wa chama cha African People’s Party of Ivory Coast (PPACI).

Hata hivyo Thiam pamoja na viongozi wengine wa upinzani, walipuuzilia mbali hatua hiyo ya Ouattara kuwania Urais.

“Tangazo la leo la Ouattara, ni ukiukaji wa katiba na demokrasia,” alisema Thiam kupitia kwa taarifa.

Duru ya kwanza ya uchaguzi huo itandaliwa tarehe 25 mwezi Oktoba.

Share This Article