Israel yasema imeanza operesheni ya ardhini kusini magharibi mwa Lebanon

Martin Mwanje
1 Min Read

Jeshi la Ulinzi la Israel limetangaza hivi punde kwamba limeanza operesheni ndogo ya ardhini dhidi ya Hezbollah katika sehemu ya magharibi ya kusini mwa Lebanon tangu jana.

Operesheni ya ardhini ya Israel kusini mwa Lebanon ilianza tarehe 30 Septemba – hadi sasa, ilikuwa imelenga upande wa mashariki wa mpaka.

IDF pia inasema ni mara ya kwanza kwa wanajeshi wa akiba wa IDF kutumika katika operesheni za mapigano kusini mwa Lebanon.

Hezbollah inasema imerusha makombora zaidi kaskazini mwa Israel

Wakati huo huo, Hezbollah inasema ilirusha makombora zaidi kaskazini mwa Israel usiku kucha.

Kundi hilo linasema lililenga maeneo yenye makombora ya Israel huko Dishon na Dalton kaskazini mwa Israel.

Pia inasema ilirusha makombora kwenye “mkusanyiko wa vikosi vya adui” huko Yir’on, makazi mengine kaskazini mwa Israel, karibu na mpaka wa Lebanon.

Mapema usiku, Hezbollah ililenga makazi ya Waisraeli magharibi zaidi, ilisema kwenye mtandao wake wa Telegraph ya lugha ya Kiingereza.

Share This Article