Israel imeapa kuendelea kufanya mashambulizi makali dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran.
Onyo hilo lilitolewa na Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz jana Jumanne.
Katz aliviambia vyombo vya habari nchini Israel kwamba kituo cha Fordow kilichopo katikati mwa Iran “bila shaka kitashughulikiwa.”
Vikosi vya Israel vimelenga vituo vingine katika mashambulizi yake, kikiwemo kile cha Natanz.
Aidha, makamanda wa Israel wamewalenga viongozi wakuu wa jeshi na maeneo ya nyuklia ya Iran.
Iran ililipiza kisasi kwa kufanya msururu wa mashambulizi yake ya makombora ambayo yameripotiwa kuwajeruhi watu 5 katikati mwa Israel.
Shirika la habari la Iran la Tasnim limeripoti kuwa awamu mpya ya mashambulizi tayari imeng’oa nanga.