Inter Milan ya Italia watapambana na PSG ya Ufaransa leo usiku katika uchanjaa wa Alianz Arena mjini Munich, Ujerumani, kuwania kombe la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Fainali hiyo itakuwa ya kwanza chini ya mfumo mpya wa ligi ya Mabingwa ulioshirikisha timu 25 katika hatua ya Makundi.
Ili kufuzu kwa fainali Inter Milan waliibandua Uhispania Barcelona ya Uhispania mabao 4-3 ,huku PSG ikiwatema Arsenal mabao 3-1 katika hatua ya nusu fainali.
Mabingwa wa leo watatia kibindoni dola milioni 27 huku watakaoshindwa wakienda nyumbani na dola milioni 20.5 za Marekani .