Ifahamu michuano ya CHAN

Kipute cha CHAN kilianzishwa mwaka 2009 na shirikisho la kandanda Afrika na hushirikisha wachezaji wanaocheza katika Ligi za Nyumbani pekee.

Dismas Otuke
2 Min Read

Makala ya nane ya fainali za CHAN yaliyopaswa kuandaliwa mwaka jana yataanza kutifua kivumbi leo katika uwanja wa kitaifa wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Tanzania, huku Taifa Stars wenyeji wakipimana ubabe na The Stallions kutoka Burkina Faso kuanzia saa mbili usiku.

Kipute cha CHAN kilianzishwa mwaka 2009 na shirikisho la kandanda Afrika na hushirikisha wachezaji wanaocheza katika Ligi za Nyumbani pekee.

Mataifa matano yametwaa ubingwa wa makala saba yaliyopita, DR Congo na Morocco wakiibuka washindi mara mbili kila moja.

Timu nyingine zilizonyakua ushindi mmoja mmoja ni Libya, Tunisia, na Senegal.

Idadi ya timu zinazoshiriki dimba la mwaka huu ni 19 kutoka kwa 16.

Kundi A

Kenya, Zambia, DR Congo, Angola, Morocco

Kundi B

Tanzania, Burkina Faso, Mauritania, Madagascar, Central African

Kundi C

Uganda, Niger, South Africa, Algeria, Guinea

Kundi D

Nigeria, Senegal, Congo, Sudan

Kwa mara ya kwanza mtambo wa VAR utatumika nchini Kenya.

Kenya ilipewa maandalia ya CHAN mwaka 2018, lakini ikalemewa na fainali hizo kuelekezwa Morocco.

Takwimu za CHAN

Kindumbwendumbwe cha CHAN chaanza leo nchini Tanzania, kabla ya mechi kuelekea Nairobi kesho kundini A.

Takwimu muhimu

Kenya na Jamhuri ya Afrika ya kati ndizo timu mbili zinaznoshirili kwa mara ya kwanza.

Mataifa 19 yanashiriki kwa mara ya kwanza.

Mshindi wa kombe hilo atatuzwa takriban shilingi milioni 450 za Kenya.

Kombe Jipya litatuza washindi.

Kenya itakuwa mwenyeji wa mechi 13, Tanzania mechi 19,na Uganda 12.

Share This Article