Wagombeaji wawili wa kiti cha ubunge cha Kasipul wametozwa faini ya shilingi milioni moja kila mmoja na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).
Philip Aroko ambaye ni mfanyabiashara na Boyd Were wa chama cha ODM, walitozwa faini hiyo baada ya kupatikana na hatia ya kukiuka sheria za uchaguzi kuhusu nidhamu.
“Wagombeaji wote wawili wamepatikana na hatia ya kukiuka sheria kadhaa za uchaguzi,” ilisema IEBC kwenye taarifa katika ukurasa wake wa X.
Wawili hao wanadaiwa kuchochea ghasia ambazo zimeshuhudiwa katika eneo bunge la Kasipul wakati za kampeni za uchaguzi.
Kwenye ghasia hizo, watu wawili wameripotiwa kufariki, huku wengi wengi wakijeruhiwa.
Baadaye, wagombeaji hao wawili walitia saini makubaliano ya kudumisha amani wakati wa kampeini wakisema wana matumaini kwamba watu wa Kasipul watafanya maamuzi yafaayo kwenye uchaguzi mdogo wa eneo hilo Nobemba 27,2025.