Vifaa vya uchaguzi vitakavyotumiwa kwenye chaguzi ndogo wiki ijayo, vitaanza kusafirishwa Ijumaa Novemba 21,2025.
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), imesema vifaa hivyo vya maeneo ya mbali kama vile eneo bunge la Banisa, vitasafirishwa kwa ndege kutokana na sababu za kiusalama.
“Usambazaji wa vifaa vya uchaguzi zikiwemo karatasi za uchaguzi, utaanza Ijumaa Novemba 21, 2025,” ilisema IEBC.
Akiongea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta alipopokea shehena ya kwanza ya karatasi za uchaguzi kutoka Ugiriki, Mwenyekiti wa tume ya, IEBC, Erastus Ethekon, aliihakikishia taifa kwamba tume hiyo iko tayari kwa chaguzi hizo ndogo za tarehe 27 mwezi huu.
Tume hiyo pia ilivialika vyama 51 vya kisiasa kushuhudia kuwasili kwa vifaa hivyo.