IEBC kuanza usajili wa wapiga kura kote nchini Jumatatu ijayo

Dismas Otuke
1 Min Read

Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC itaanza zoezi la kuwasajili wapiga kura kote nchini Jumatatu ijayo, Septemba 29.

IEBC itawaruhusu wapiga kura kujisajili au kubadilisha vituo vya kupigia kura kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Kulingana na taarifa ya IEBC, zoezi hilo litaandaliwa katika maeneo bunge yote nchini isipokuwa yale yatakayokuwa na uchaguzi mdogo.

IEBC inalenga kutumia zoezi hilo kuwa na taarifa za kutosha kuhusu idadi ya wapiga kura nchini.

TAGGED:
Share This Article