Idadi ndogo ya wapiga kura yashuhudiwa Mbeere Kaskazini

Tom Mathinji
2 Min Read

Idadi ndogo ya wapiga kura imeshuhudiwa katika eno bunge la Mbeere Kaskazini, huku chaguzi ndogo zikitekelezwa kote nchini.

Katika kituo cha kupiga kura cha shule ya msingi ya Kanyuambora, maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), walifungua milango ya kituo hicho saa kumi na mbili asubuhi, huku wakazi wakivumilia kibaridi cha asubuhi na kupanga foleni za kupiga kura.

Aliyekuwa Waziri wa Utumishi wa Umma Justin Muturi, alipiga kura yake katika kituo hicho cha kanyauambora.

Muturi ambaye pia ni kiongozi wa chama cha Democratic Party (DP), aliwahimiza wakazi wa Mbeere Kaskazini kupiga kura kwa utulivu na kudumisha amani.

Spika huyo wa zamani wa Bunge la Taifa, alielezea matumaini kwamba muwaniaji wa chama hicho Newton Karish ataibuka mshindi.

Mwaniaji wa kiti cha eneo bunge la Mbeere Kaskazini Leonard Wamuthende akipiga kura katika kituo cha Siakago Social hall.

Mwaniaji wa kiti hicho wa chama cha UDA Leonard Wamuthende, alipiga kura yake katika kituo cha kupiga kura cha Siakago Social hall, akiwa ameandamana na Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku.

Wamuthende aliwasihi wafuasi wake kudumisha amani wakati wa zoezi hilo.

Kutoka hapo nilifululiza hadi kituo cha kupiga kura katika shule ya msingi ya Gitiburi ambako Waziri Ruku naye alipiga kura yake.

Mwaniani wa eneo bunge la Mbeere Kaskazini wa chama cha DP Newton Karish apiga kura katika kituo cha kupiga kura cha Karambari.

Mwaniani wa chama cha Democratic Party  Newton Karish, naye alipiga kura katika kituo cha upigaji kura cha shule ya Karambari wakilishi wadi ya Muminji.

Kiti cha eneo bunge la Mbeere Kaskazini kiliachwa wazi baada ya aliyekuwa mbunge wa eneo hilo, Geoffrey Ruku kuteuliwa katika Baraza la Mawaziri.

Share This Article