ICC yatoa vibali vya kukamatwa kwa viongozi wawili wa Taliban

Tom Mathinji
1 Min Read
Mahakama ya ICC yatoa vibali vya kukamatwa kwa viongozi wawili wa Taliban.

Mahakama ya kimataifa ya kushughulikia kesi za jinai imetoa vibali viwili vya kukamatwa kwa viongozi wa wawili wakuu wa kundi la Taliban dhidi ya uhalifu wa kibinadamu kwa kuwatesa wanawake na wasichana nchini Afghanistan.

Mahakama hiyo imesema zipo sababu za kuamini kuwa kiongozi mkuu Haibatullah Akhundzada na jaji mkuu  Abdul Hakim Haqqani waliongoza kampeni ya ukandamizaji wa kijinsia tangu kundi hilo lilipochukua mamlaka mwaka 2021.

Chini ya utawala wao, wasichana wa umri wa miaka 12 walipigwa marufuku ya kwenda shuleni,nao wanawake wakizuiliwa kufanya kazi na kuwekewa vikwazo vya usafiri  na kuzungumza kuhusu maswala fulani.

Mahakama ya  ICC imesema sera hizi zililenga wanawake na wasichana  na kuwanyima haki za kimsingi hali ambayo umoja wa mataifa imetaja kuwa ubaghuzi wa kijinsia.  Kundi la Taliban hatahivyo limesema sera zake zinaashiria utamaduni wa Afghan na sheria ya kiislamu.

Lakini kundi la wanaharakati limekaribisha hatua ya mahakama hiyo, wakiimiza hatua zaidi .

 

TAGGED:
Share This Article