Hospitali ya rufaa na mafunzo ya Jaramogi Oginga Odinga yapandishwa hadhi

Katibu wa huduma za matibabu Dkt Ouma Oluga ametangaza haya leo Jumatatu alipofanya ziara hospitalini humo, akiitaja kuwa yenye uwezo mkubwa wa kutoa huduma bora.

Dismas Otuke
1 Min Read

Hospitali ya rufaa na mafunzo ya Jaramogi Oginga Odinga (JOORTH) imepandishwa cheo kutoka kiwango cha 6 hadi kiwango cha C5, kiwango ambacho awali kilitengewa  vyuo vikuu vya umma.

Katibu wa huduma za matibabu Dkt Ouma Oluga ametangaza haya leo Jumatatu alipofanya ziara hospitalini humo, akiitaja kuwa yenye uwezo mkubwa wa kutoa huduma bora.

Oluga aliongeza kuwa kupandishwa hadhi kwa hospitali hiyo kutaiweka katika nafasi bora ya kuwaajiri wahudumu wa afya waliohitimu na pia kuweza kuwazuia kuhamia hospitali nyingine.

Share This Article