Waziri wa Afya Deborah Barasa ametangaza kuwa serikali itaanza kulipa malipo ya SHA kwa hospitali zilizotoa huduma za matibabu kwa wagonjwa kuanzia mwishoni mwa mwezi huu.
Licha ya kubadilishwa kwa bima ya hospitali kutoka NHIF hadi bima mpya ya SHIF Oktoba mosi na kuanza kutekelezwa kwa makato mapya, Wakenya wengi wamekuwa wakilalama kwa kukosa huduma hospitalini hadi sasa.
Barasa amesema tayari wizara yake imelipia shilingi bilioni 5 kati ya bilioni 19, huku kiwango kingine cha bilioni 2.5 kikitarajiwa kulipwa kufikia mwishoni mwa wiki hii.
Waziri amesema haya leo alipozuru hospitali ya rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga katika kaunti ya Kisumu kukagua maendeleo ya usajili wa huduma ya bima ya SHA.