Highways yahifadhi taji la soka ya Nairobi

Dismas Otuke
1 Min Read

Shule ya upili ya Highway imenyakuwa tena taji la soka baina ya shule za upili eneo la Nairobi baada ya kulaza washindani wao wa mwaka jana – Olympic mabao mawili kwa sufuri kwenye fainali iliyosakatwa katika shule ya Nairobi wikiendi hii.

Mabao hayo yalitingwa katika kipindi cha pili kupitia usaidizi wa mchezaji bora wa mchezo huo Rial Biliew.

Katika soka ya akina dada, mambo yalikuwa vile vile, baada ya mabingwa watetezi Dagorreti kuwalambisha sakafu wenzao wa Soweto goli moja kwa bila.

Kufuatia ushindi huo, timu hizo zitawakilisha eneo la Nairobi katika mashindano ya kitaifa mjini Kakamega kuanzia tarehe 29 mwez huu.

Timu zingine zitakazowakilisha Nairobi ni wavulana wa Upper Hill na vipusa wa Bururu waliotamba katika mchezo wa vikapu wa wachezaji watatu kila upande, Warembo wa Soweto na wavulana wa Ruthimitu waliofana kwenye voliboli, wasichana wa Caren C na wavulana wa Lenana waliofaulu kwenye raga ya wachezaji saba kila upande.

Iwapo timu hizo zitafaulu awamu hiyo, zitashiriki mashindano ya Afrika Mashariki baina ya shule za upili yatakayoandaliwa pale pale Kakamega.

TAGGED:
Share This Article