Helikopta ya kijeshi imeanguka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aden Adde mjini Mogadishu Jumatano asubuhi, kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa vyombo vya habari vya ndani.
Picha zilizosambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha moshi mzito ukipanda kutoka uwanja wa ndege, unaoripotiwa kusababishwa na moto uliozuka kufuatia ajali hiyo.
Kufikia sasa, hakuna taarifa rasmi zilizotolewa na mamlaka ya uwanja wa ndege au serikali ya shirikisho kuhusu sababu ya ajali hiyo, kiwango cha uharibifu, au umiliki wa ndege inayohusika.
“Tulisikia mlipuko mkubwa na kuona mosi ukifuka juu ya helikopta. Hatukujua kama ilikuwa ikipaa au ikitua,” alisema aliyeshuhudia ajali hiyo.