Timu ya Harambee Stars imewasili mjini Arusha, Tanzania, kushiriki mashindano ya kimataifa ya mataifa manne kujiandaa kwa fainali za nane za Kombe La CHAN.
Kenya itachuana na Uganda katika mechi ya kwanza Jumatatu ijayo kabla ya kukabiliana na wenyeji Taifa Stars siku tatu baadaye kisha ifunge ratiba dhidi ya mabingwa watetezi wa CHAN Senegal Julai 27.
Harambee Stars imejumuishwa kundi A katika fainali za CHAN pamoja na Angola, Zambia, DR Congo na Morocco huku wakifungua ratiba dhidi ya Congo Agosti 3 katika uwanja wa Kasarani.
Kikosi cha Kenya kilichosafiri kuelekea Arusha kinawajumuisha: Makipa, Faruk Shikhalo, Byrne Omondi na Sepstanios Wekesa, wakati walinzi wakiwa Siraj Mohammed, Manzur Suleiman, Rwamba Swaleh, Abud Omar, Alphonce Omija, Sylvester Owino, Michael Kibwage, Daniel Sakari, Lewis Bandi na Kevin Okumu.
Kiungo cha kati kinasheheni Apha Onyango, Abud Omar, Marvin Nabwire, Austine Odhiambo, Ben Stanley na Boniface Muchiri.
Washambulizi ni Mohammed Bajaber, David Sakwa, Ryan Ogam, Felix Oluoch, Austin Odongo na Masud Juma.