Harambee Stars yajihakikishia angalau shilingi milioni 25.8 kwa CHAN

Timu zitakazomaliza nafasi za tatu  katika makundi ya A, B, na C zitapokea shilingi milioni 38.7 kila moja,huku zile za mwisho zikiondoka na shilingi milioni 25.8 kila moja.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa Harambee Stars imejihakikishia kupokea angalau shilingi milioni 25.8, kwa kushiriki makala ya nane ya kipute cha kombe la Afrika kwa wachezaji wa Ligi za nyumbani (CHAN) kati ya Agosti 2 na 30 mwaka huu katika mataifa ya Uganda, Tanzania, na Kenya.

Kwa mujibu wa viwango vya zawadi ya pesa vilivyotangazwa na shirikisho la soka Afrika (CAF), shilingi bilioni 1.3 ni ongezeko la asilimia 32 kutoka kwa shilingi bilioni 1.02 zilizotuzwa katika makala yake mwaka 2022 nchini Algeria.

Mabingwa watatuzwa shilingi milioni 452.2, za Kenya, nafasi ya pili milioni 155, huku timu ya tatu ikienda nyumbani na shilingi milioni 90.4.

Timu zitakazomaliza nafasi za tatu  katika makundi ya A, B, na C zitapokea shilingi milioni 38.7 kila moja,huku zile za mwisho zikiondoka na shilingi milioni 25.8 kila moja.

Timu zitakazofika robo fainali zitatapokea shilingi milioni 58.1 kila moja.

Kenya watafungua dimba ya CHAN kundini A dhidi ya DRC Jumapili ijayo katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani.

Tanzania watafungua kipute hicho tarehe 2 mwezi ujao katika uwanja wa kitaifa wa Benjamin Mkapa mjini Dares Salaam.

Share This Article