Harambee Stars wameimarisha mazoezi yao kujiandaa kwa mechi ya ufunguzi ya kuwania Kombe la CHAN kundini A, dhidi ya DR Congo, Jumapili hii katika uwanja wa Kasarani.
Aidha, mshambulizi wa Shabana FC Brian Michira, alijiunga na kambi jana sawia na Chris Erambo wa Tusker FC, na Edward Omondi wa Sofapaka FC.
Kocha Mkuu Benni McCarthy, alilazimika kufanya mabadiliko hayo kutokana na majeruhi wengi kikosini akiwemo kiungo mkabaji Mohammed Bajaber wa Police FC ambaye huenda akose fainali hizo.
Msanii maarufu wa muziki humu nchini Bien Aime Baraza alitembelea kambi ya mazoezi ya Kenya jana na kuwatia shime wachezaji.
Timu nyingine kundini A pamoja na Kenya ni Zambia, Angola, na Morocco.