Timu ya taifa ya soka Harambee Stars, imeendeleza mazoezi yake leo katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo kujiandaa kwa makala ya nane, ya fainali za kombe la CHAN itakaposhiriki kwa mara ya kwanza.
Kinara wa shirikisho la kandanda nchini Hussein Mohammed, akizuru kambi hiyo, alielezea Imani yake kuwa itasajili matokeo mazuri wakati wa kipute cha CHAN.
Kenya wamerejea mazoezini baada ya kujiondoa kwa mechi za CECAFA za mataifa manne zinazoendelea mjini Arusha, Tanzania.
Kenya itafungua mechi za kundi A tarehe 3 mwezi ujao dhidi ya mabingwa mara mbili, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo.
Mataifa mengine kundi A pamoja na Kenya ni mabingwa mara mbili Morocco, Angola na Zambia.