Harambee Stars yaelekea Uturuki kwa mechi za kirafiki

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya soka ya Kenya ,Harambee Stars imeondoka nchini leo kuelekea Uturuki inakotarajiwa kucheza mechi mbili za kujipima nguvu dhidi ya Equitorial Guinea na Senegal kuanzia mwishoni mwa juma hili.

Harambee Stars imeratibiwa kukabiliana na Equitorial Guinea tarehe 14 mwezi huu kwa mchuano wa kwanza wa kirafiki kabla ya kumenyana na Senegal Novemba 18.

Itakuwa mara ya kwanza kwa Kenya kuchuana na Senegal tangu mwaka 2004 wakati  Simba hao wa Teranaga walipoizaba Harambee Stars mabao 3-0 katika mechi ya kombe la AFCON.

Share This Article