Harambee Stars wajiondoa mechi za kirafiki za CECAFA katika hali tatanishi

Hatua hii ina maana kuwa ni timu za Tanzania, Burkina Faso na Uganda pekee zitakazoshiriki mechi hizo za kirafiki.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa Harambee Stars imejiondoa kwa michuano ya kirafiki ya CECAFA ya mataifa manne, iliyokuwa ianze leo mjini Arusha, Tanzania.

Licha ya shirikisho la FKF kusema kuwa timu hiyo iliondolewa kutokana na mazingira mabovu, kuna maswali mengi kuliko majibu kuhusu maamuzi duni ya usimamizi wa timu kuhusu mashindano hayo.

Kenya ilipangiwa kufungua mechi hizo za kirafiki dhidi ya Uganda leo jioni.

Hatua hii ina maana kuwa ni timu za Tanzania, Burkina Faso na Uganda pekee zitakazoshiriki mechi hizo za kirafiki.

Harambee Stars itaanza kampeni ya CHAN tarehe 3 mwezi ujao dhidi ya DR. Congo, nechi ya kundi A, katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani.

Timu nyingine kundini humo ni Morocco, Zambia na Angola.

Harambee Stars ilwiasili Arusha mapema Jumamosi kujiandaa kwa mechi hizo za kujipima nguvu.

Share This Article