Timu ya tafa ya soka ya Kenya, Harambee Stars ililazimisha sare ya bao moja katika mchuano wa pili wa kundi A kuwania kombe la CHAN, uliopigwa katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani jana usiku.
Kenya ililazimika kucheza kwa takriban dakika 80 ikiwa na wachezaji kumi baada ya Marvin Nabwire, kulishwa kadi nyekundu,wakiwa na wakati mgumu kuzima mashambulizi ya Angola.
Palancas Negras walianza kwa kasi huku wakichukua uongozi kupitia kwa Paciencia ,katika dakika ya saba.
Kenya ilisawazisha dakika tano baadaye wakati mshambulizi Austin Odhiambo, alipounganisha penati baada yake kuangushwa na beki Mafuta.
Kiungo mkabaji Marvin Nabwire alitimuliwa uwanjani kwa kupigwa kadi nyekundu kwa kucheza ndivyo sivyo katika dakiak ya 21.
Kenya inaongoza kundi A kwa pointi 4,ikifatwa na Morocco na DR Congo kwa alama sawia tatu, huku Angola ikiwa ya nne kwa alama 1.
Harambee Stars itarejea Kasarani Jumapili hii dhidi ya Morocco kuanzia saa tisa alasiri.