Timu ya taifa ya soka ya Kenya harambee Stars itakabiliana na Gambia na Ushelisheli katika mechi mbili muhimu za kundi F kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka ujao.
Kenya chini ya ukufunzi wa Benni McCarthy itachuana na Gambia Ijuamaa Septemba 5, katika uwanja wa Kasarani kuanzia saa kumi jioni .
Baadaye Kenya itawaalika Ushelisheli Jumanne ijayo tarehe 9 Septemba kwa mchuano mwingine katika uga uo huo wa Kasarani.
Kikosi cha Harambee Stars kinawajumuisha wachezaji 13 walioshiriki fainali za CHAN maajuzi na wale wa kulipwa.
Kenya ni ya nne katika kundi hilo kwa pointi 6 ,nyuma ya viongozi Gabon walio na alama 18 ,wakifuatwa na Ivory Coast walio na alama 16 huku Burundi ikiwa na alama 10.
Harambee Stars hawana budi kushinda mechi hizo ili kufufua matumaini ya kufuzu kwa kombe la dunia kwa mara ya kwanza.