Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars, leo jioni itamenyana na Senegal, maarufu kama Teranga Lions, katika mechi ya kimataifa ya kirafiki itakayosakatwa nchini Uturuki.
Pambano hilo litarushwa mubasahara na runinga ya KBC.
Ni mara ya kwanza kwa Kenya kuchuana na Senegal tangu kwenye fainali za AFCON mwaka 2004 wakati Kenya ilizabwa magoli 3-0.
Senegal ni ya 18 kwenye msimamo wa dunia na ya pili bora Afrika baada ya Morocco, huku Kenya ikikalia nambari ya 111 kulingana na msimamo wa mwezi jana wa FIFA.
Harambee Stars wanacheza mchuano wa leo baada ya kulazwa bao moja bila wiki jana na Equatorial Guinea.