Timu ya taifa ya soka Harambee Stars itashiriki fainali za CHAN kuanzia tarehe 2 hadi 30 mwezi ujao, bila huduma za wachezaji nyota wa Ligi Kuu msimu uliomalizika.
Kocha mkuu wa Harambee Stars Benni McCarthy, amelazimika kuwaita kambini wanandinga wengine baada ya kiungo mkabaji Mohammed Bajaber wa Police FC kuondoka kikosini Jumatatu, kujiunga na miamba wa Tanzania Simba, walio kambini nchini Misri.
Yamkini Bejaber aliye na umri wa miaka 22, amesaini mkataba wa miaka mwili na wekundu wa msimbazi Simba.
Harambee Stars pia itazikosa huduma za mfungaji bora wa ligi kuu msimu jana, Moses Shumah wa Kakamega Homeboyz, ambaye amejiunga na klabu ya Power Dynamos ya Zambia.
Shumah aliongoza chati ya ufungaji mabao katika ligi kuu ya Kenya msimu wa mwaka 2024/2025, kwa jumla yaa magoli 17.
Aidha, mfungajii bora wa pili Emmanuel Osoro wa Talanta FC, aliyepachika mabao 16 msimu jana, alijiondoa kikosini baada ya kusainiwa na Dynamos ya Zambia kwa kondrati ya miaka miwili.