Timu ya taifa ya soka ya Kenya itaondoka nchini kesho kuelekea Arusha, Tanzania, kwa mechi za mataifa manne kujipiga msasa kwa fainali za kombe la CHAN.
Kenya itacheza mchuano wa ufunguzi dhidi ya Uganda Jumatatu ijayo.
Mataifa mengine kwenye mechi hizo za kirafiki ni Tanzania na mabingwa watetezi wa CHAN, Senegal.
Harambee Stars watafungua makala ya nane ya kipute cha CHAN Agosti 3 dhidi ya DR Congo, katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani kundini B.
Stars chini ya ukufunzi wa Benni McCarthy imekuwa kambini katika uwanja wa Kasarani kujiandaa kwa CHAN.