Harambee Starlets yawasili Dar, kwa CECAFA

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya ya wanawake Harambee Starlets,iliwasili Dares Salaam jana jioni tayari kushiriki makala ya mwaka huu ya michuano ya CECAFA nchini Tanzania.

Starlets chini ya kocha Beldine Odemba, itarumia michuano hiyo kwa maandalizi ya mechi zakufuzu fainali za kombe la mataifa ya Africa WAFCON mwaka ujao nchini Morocco.

Kenya itafungua kampeni yake dhid ya Burundi Jumapili Juni 15.

Starlets watakabiliana na Gambia, katika mechi ya kufuzu WAFCON Septemba mwaka huu.

Wenyeji Tanzania watamenyana na Sudan Kusini huku Uganda ikichuana na Burundi katika mechi za ufunguzi kesho.

Kikosi
Makipa
Annedy Kundu, Lilian Awuor, Vivian Shiyonzo

Mabeki
Elizabeth Ochaka, Alice Mideri, Tabitha Amoit, Janet Mumo, Ruth Ingosi, Dorcas Shikobe, Enez Mango, Vivian Nasaka

Viungo
Diana Wacera, Martha Amunyolet, Fasila Adhiambo, Lavender Ann Akinyi, Medina Abubakar Hussein, Corazone Aquino

Washambulizi
Emily Morang’a, Swaum Nanjaka Masungo, Faith Mboya, Elizabeth Wambui, Tumaini Waliaula, Violet Nanjala

Share This Article