Timu ya taifa ya soka ya akina dada Harambee Starlets iliwasili nchini mapema leo kutoka Tunisia, ilikosajili ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya wenyeji na kufuzu kwa raundi ya pili na ya mwisho.
Starlets chini ya ukufunzi wa kocha Beldine Odemba, ilipokelewa katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta, na Rais wa shirikisho la soka nchini FKF Hussein Mohammed.
Kenya itamenyana na Gambia mwezi oktoba mwaka huu katika raundi ya pili huku mshindi akijikatia tiketi kucheza fainali za kuwania kombe la mataifa ya Afrika (WAFCON) mwaka ujao.
Starlets waifuzu kwa mra ya kwanza na ya mwisho kwa kipute cha WAFCON mwaka 2016.