Harambee Starlets wajikaanga na kuwapa Twiga Stars kombe la CECAFA

Bao la kujifunga la dakika ya 49 lake beki Enoz Mango, lilitosha kuwapa Tanzania kombe la tatu na la kwanza tangu mwaka 2018.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wenyeji Twiga Stars kutoka Tanzania ndio mabingwa wa Kombe la CECAFA ,kwa mara ya tatu katika historia baada ya kuilaza Harambee Starlets ya Kenya bao moja kwa bila.

Mchuano huo wa mwisho ulisakatwa Jumamosi jioni katika uwnaja wa Azam Compplex jijini Dares Salaam.

Bao la kujifunga la dakika ya 49 lake beki Enoz Mango, lilitosha kuwapa Tanzania kombe la tatu na la kwanza tangu mwaka 2018.

Tanzania walishinda mechi zote nne na kuongoza kwa alama 12 huku Kenya wakishinda mchuano mmoja.

Mabingwa wa mwaka 2022 Uganda walimaliza katika nafasi ya tatu.

Share This Article