Timu ya taifa ya soka ya Kenya ya wanawake ya Kenya,Harambee Starlets, imesajili ushindi wa pili kwenye Makala ya mwaka huu ya kuwania Kombe la CECAFA nchini Tanzaznia baada ya kuwatitiga mabingwa watetezi Uganda mabao 4-0 Jumanne jioni.
Kiungo Diana Wacera alipachika goli la kwanza kunako dakika 19, kabla ya Dorcas Sikobe, kuongeza la pili dakika nane baadaye kisha Violet Wanyonyi, akapachika la tatu dakika ya 29 ,Kenya wakiongoza tatu bila kufikia mapumzikoni.
Martha Amunyolet alitikisa nyavu dakika ya 80, huku Kenya wakipata ushindi mnene dhidi Crested Cranes wakiweka hai matumaini ya kufuzu wa fainali ukiwa ushindi wa pili.
Kenya wanaonolewa na kocha Beldine Odemba ,watashuka uwanjani kwa mchuano wa tatu dhidi ya Sudan Kusini kesho kutwa,kabla ya kufunga ratiba dhidi ya wenyeji Tanzania maarufu kama Twiga Stars.
Kenya na Tanzania wanaongoza msimamo kwa alama sawa sita kila moja,wakifuatwa na Burundi na Uganda kwa ponti 3 kila moja.
Tanzania iliwanyuka Sudan Kusini mabao 6 kwa nunge.