Gor Mahia yafurusha wakufunzi wote

Mwenyekiti wa Gor, Ambrose Rachier, alitangaza jana kuwa wamesitisha mikataba yote ya maafisa wa benchi ya kiufundi .

Dismas Otuke
1 Min Read

Waliokuwa mabingwa wa Ligi Kuu Gor Mahia, wamefanya mabadiliko makubwa  ya uongozi katika jitihada za kuifufua timu hiyo.

Mwenyekiti wa Gor, Ambrose Rachier, alitangaza jana kuwa wamesitisha mikataba yote ya maafisa wa benchi ya kiufundi .

Aidha Rachier alifichua kuwa wanapania kumteua mkufunzi mpya na wasaidizi wake hivi karibuni.

Kocha mkuu Zedekiah Zico Otieno na  wasaidizi walifurushwa kufuatia msururu wa matokeo mabovu msimu uliomalizika.

Gor walimaliza katika nafasi ya pili Ligini na pia wakamaliza wa pili katika kombe la FKF, hatua inayowaacha nje ya taji lolote la Afrika msimu ujao.

Share This Article