Gharama ya maisha kupanda baada ya bei za mafuta kuongezwa

Tom Mathinji
1 Min Read
EPRA yadumisha bei za Mafuta.

Wakenya watalazimika kugharimika zaidi baada ya bei za mafuta kupanda katika tathmini mpya iliyotangazwa na Halmashsauri ya Kudhibiti bei za Nishati na Mafuta (EPRA) siku ya Jumatatu.

Kulingana na tathmini hiyo, bei hizo mpya zitaanza kutekelezwa Julai 15 hadi Agosti 14, 2025.

Kwenye taarifa ya EPRA, bei ya lita moja ya  Super petrol imeongezeka kwa shilingi 8.99, mafuta taa kwa shilingi 8.67 huku dizeli ikiongezeka kwa shilingi 9.65.

Jijini Nairobi, lita moja ya mafuta ya Super Petrol itauzwa shilingi 186.31, dizeli itauzwa shilingi 171.58, nayo bei ya mafuta taa kuuzwa kwa shilingi 156.58.

Mjini Mombasa, lita moja ya Super Petrol huku dizeli na mafuta taa ikiuzwa kwa shilingi 183.02, 168.30 na 153 mtawalia.

Jijini Kisumu, wateja watanunua lita moja ya Super Petrol kwa shilingi 186.15, dizeli shilingi 171.78 na mafuta taa shilingi 156.83.

TAGGED:
Share This Article